Wanaume wengi wanatamani kuongeza urefu na upana wa maumbile
yao ya uzazi, kutokana na kuathirika kisaikolojia kunakowafanya waamini
mabadiliko hayo huongeza uwezo wa kumfikisha mwenza kileleni.
Vilevile, wanaume hawa huamini maumbile hayo yanayoleta
msisimko kupita kiasi na wakiwa nayo wataonekana marijali na watawavutia
wanawake walionao.
Wanafanya hivi kwa kukosa uelewa kuwa msisimko na kilele cha
tendo la ndoa unatokana na ujuzi binafsi, kwa kutumia akili na viungo vya mwili
kuleta na kuongeza msisimko baina ya wenza waliotayari.
Wasichokijua ni kwamba kinachotakiwa ni kuwa na uume wa
wastani kuliko mkubwa uliopitiliza unaoweza kuwasababishia maumivu wenza wao,
jambo litakalofanya mwisho wa siku wasifurahie tendo hilo na kuongeza uwezekano
wa kupata hofu kutokana na ukubwa huo.
Laiti kungelikuwa na njia salama za kunenepesha na kurefusha
maumbile katika huduma rasmi za afya, gharama za kuchangia matibabu zingekuwa
maradufu. Kwa sababu wanaume wengi
wanaodhani wana maumbile madogo ya uume wangemiminika kwenda kutibiwa tatizo
hilo.
Mamlaka za ndani za kimataifa kama vile Wizara ya Afya,
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na
vyuo vikuu vilivyobobea kufanya utafiti kikiwamo Havard, hakuna mahala ambapo
wamepitisha na kupendekeza dawa au kifaatiba kwa ajili ya huduma hiyo.
Watu wanene kupitiliza, shina la uume lililo chini ya kitovu
humezwa na mafuta na nyama zilizorundikana hapo, hivyo hupunguza urefu wa
kiungo hicho muhimu kwa tendo la ndoa.
Zipo njia chache ambazo jumuia za kimataifa na mamlaka za
afya wanakubali kuwa zinaweza kusaidia angalau kuongeza urefu, lakini usiozidi
nchi moja, njia hizo ni pamoja na kupunguza unene.
Hivyo, kupunguza unene kwa njia ya vyakula na mazoezi
inakubalika. Vilevile kwa njia ya
upasuaji kwa lengo la kupunguza mafuta ya eneo hilo inakubalika pia.
Vitu vinavyotumika kiholela kunenepesha na kurefusha uume ni
pamoja na vidonge, sindano, virutubisho, mashine maalumu, upasuaji wa
kupandikiza, vifaa vya mazoezi ya uume, mafuta ya kupaka uumeni na mitishamba.
Vitu hivi vinauzwa kisiri katika baadhi ya maduka ya dawa,
kwa njia ya mtandao, kutembezwa mtaani au matangazo kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.
Lakini, kati ya hivyo nilivyovitaja, hakuna vinavyofanya
kazi kwa ufanisi na kukidhi vigezo vya kitaalam kupitia vyombo vikubwa vya
matibabu na uthibiti wa magonjwa ikiwamo WHO.
Kwa sababu hakuna utafiti wa kisayansi kuthibitisha ubora,
ufanisi na usalama wa vifaatiba hivyo au njia zilizopendekezwa ingawa ni kweli,
vipo baadhi ambavyo kwa muda mfupi, vinaweza kukusaidia lakini vikikuacha na
madhara makubwa hapo baadae.
Madhara hayo ni pamoja na kupungua au kukosa kabisa nguvu za
kiume, kuchubuka uumeni, kuvunjika kwa misuli sponji ya uume, madhara ya nerve
na kupata maumivu sugu wakati wa kujamiiana.
Taarifa zinaonesha wanaume wengi wao kwenda kwenye kituo cha
huduma za afya au hospitali kwa ajili ya uchunguzi na ushauri. Wengi wanaojihisi wana uume mdogo hugundulika
kuwa hawapo chini ya nchi tatu baada ya uume kusimama.
No comments:
Post a Comment