Wengi hutumia pilipili hoho kwenye mapishi ya aina
mbalimbali bila kufahamu wingi wa vitamin zilizomo pamoja na uwezo wake
kuboresha mifumo mbalimbali ya mwili.
Pilipili za rangi ya njano zinaongoza kwa wingi wa
virutubisho vya zeaxanthin zikifuatiwa na mahindi. Hata hivyo, pilipili hoho au sweet
pepper zina uwezo wa kuongeza kinga ya mwili pamoja na kupambana na
magonjwa ya saratani, moyo hukusaidia kuboresha uwezo wa macho kuona vizuri.
Matumizi yake yanahusisha kiungo cha mboga au sehemu muhimu
ya kachumbari na kutengeneza juisi ambayo husaidia kutoa takamwili, yanairuhusu
itumike wakati wowote na kumfurahisha mlaji.
Hoho hupatikana katika muonekano wa rangi tofauti ambazo ni
rangi nyekundu, kijani, urujuani na njano na inatajwa kuwa ni mboga yenye
vitamin zaidi ya 30.
Miongoni mwa faida zilizopo katika hoho ni uwezo wake wa
kutibu muwasho wa vidonda vya kooni, kutoa damu puani na kuimarisha kinga ya
mwili kutokana na wingi wa vitamin C iliyonayo.
Hoho husaidia watu wenye shida katika mfumo wa upumuaji kutokana na kuwa
na vitamin C nyingi, hukinga dhidi ya magonjwa ya saratani ya kibofu cha mkojo
na ugonjwa wa baridi yabisi.
Husaidia kupunguza uzito, kuboresha mzunguko wa damu na
kupunguza lehemu mwilini kutokana na kiwango kidogo cha kalori ilichonacho
pamoja na kuzuia shinikizo la damu na kutibu anemia.
Hutibu kuhara, ugonjwa wa homa ya manjano, hurekebisha
presha ya kupanda na husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi
vizuri. Kwa wanaosumbuliwa na gesi
tumboni wanashauriwa kutengeneza juisi ya pilipili hoho wakichanganya na
spinachi kumaliza tatizo hilo.
Zipo pilipili hoho zenye rangi ya njano ambazo zikitumika
katika mapishi ni mboga yenye faida nyingi kiafya. Zinauwezo wa kuboresha mifumo mbalimbali
mwilini zikiwa na wingi wa zeaxanthin kuliko mboga nyingine. Hata hivyo, watalaam wa masuala ya afya
wanasema hoho rangi ya njano ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya lutein na
zeaxanthin ambazo huzuia matatizo ya mtoto wa jicho na udhaifu wa misuli.
Pilipili hoho za rangi nyekundu inabaki ina
kirutubisho cha lycopene ambacho hupunguza hatari ya saratani mbalimbali.
No comments:
Post a Comment