Moja ya jambo ambalo huwaumiza kichwa wanaume wengi ni kuwa
na maumbile madogo ya kiume. Wengi
huamini uume mrefu na mpana ndiyo urijali wenyewe kuweza kumfikisha kileleni
mwanamke.
Wanasayansi wengi wa tiba wametoa machapisho mengi ya
kitafiti kuhusu urefu na upana wa uume juu ya wastani unaokubalika.
Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiishi kwa hofu na kukosa
kujiamini katika mahusiano yao kwa kuhisi wana uume mdogo usioweza kumridhisha
mwenza.
Hofu hiyo inawezekana ni kutokuwa na ufahamu sahihi juu ya maumbile yao yanavyotakiwa
kuwa. Wengi wanakosa taarifa sahihi
kutoka kwa wataalam wa afya wenye uelewa wa kutosha wa jambo hili.
Hofu ya wanaume inapanda zaidi kila siku kutokana hasa na
utitiri wa matangazo ya magazeti, mitandaoni, stori za vijiweni na matangazo ya
matabibu wa mtaani wanaojitangaza kuwa na dawa na vifaatiba vya kukuza uume.
Dondoo zifuatazo zinajumuisha machapisho ya kitafiti
yakiwamo yaliyochapishwa katika majarida makubwa na maarufu duniani kama vile
Science Today, Men’s Health na British Journal of Urology International.
Asilimia 85 ya wanawake wanaridhika na urefu na upana wa
maumbile ya uume wa wenza wao ingawa wanaume wenyewe hawana uhakika wa jambo
hilo huku asilimia 45 ya wanaume wanaamini wana maumbile madogo.
Utafiti unahitimisha kuwa wastani wa urefu wa uume ukiwa
tepetepe yaani kabla ya kusimama ni kati ya sentimita saba mpaka 10 au inchi
2.8 hadi 3.9. urefu huu unapimwa kuanzia kwenye shina la uume mpaka kichwani.
Urefu wa uume unapokuwa umesimama ni kati ya sentimita 12 na
16 au inchi 4.7 hadi 6.3. urefu wa
mzunguko wa uume ukiwa umesimama ni kati ya sentimita 12 au inchi 4.7.
Dondoo nyingine zinaonesha wanaume wenye unene uliopitiliza
na wenye umri mkubwa wengi wao wana urefu mfupi wa uume ukiwa umesimama.
Maumbile ya uume yanatofautiana kati ya jamii moja na
nyingine, bara moja na jingine. Wanaume
wanaotokea Asia wana maumbile madogo ya uume ukilinganisha na wanaume wa
Afrika.
Wanawake wengi huwa hawajali urefu na upana wa uume wa wenza
wao pengine kutokana na ukweli kuwa kufika kilele cha tendo kwa wanawake si
lazima kumuingilia, wanaweza kufanya hivyo hata kwa kutomaswa tu au njia
nyinginezo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Ernst Grafenberg wa
Ujerumani aligundua sehemu muhimu inayoelezwa kuwa na msisimko wa kipekee
kuliko nyingine yoyote katika sehemu za kike.
Sehemu hiyo ijuliknayo kama G-spot ambayo ipo sentimita
5.1-7.9 au inchi 2-3 tu kuanzia nje ya uke kuingia ndani.
Inaelezwa, unaweza kuwa na uume mdogo lakini ukamridhisha
mwenza wako na kumfikisha kileleni ukiweza kuisisimua sehemu hiyo.
Wanaohisi kuwa na maumbile madogo wasikimbilie
dawa za mtaani kwani utapeli ni mwingi bali waende kwa watoa huduma za kisasi
za afya zinazotambulika kwa ajili ya ushauri.
No comments:
Post a Comment