Bamia ni miongoni mwa mboga ambazo baadhi huziona ni za
kawaida wanapozitumia kwenye milo yao.
Licha ya kuwa mboga, bamia ina faida nyingi mwilini na
kiuchumi. Hulimwa maeneo yenye joto,
ukanda wa kitropiki ikiwamo maeneo makavu.
Miongoni mwa faida zake mwilini ni kusaidia kuondosha vimelea vya sumu
kwenye ngozi.
Vilevile, inasaidia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza
kinga ya mwili. Bamia ina kiasi kikubwa
cha vitamin C, K na folic acid ambayo husaidia mmeng’enyo wa chakula.
Wenye kisukari au wenye majeraha wanashauriwa kula bamia kwa
wingi kwani ina mchango katika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu pamoja
na kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.
Ina vitamin A ambayo husaidia kutengeza kinga ya dhidi ya
maradhi na sumu za aina ambazo zinaweza zikaingia mwilini. Mbali na hayo, bamia husaidia kulainisha choo
na kuongeza hamu la kula.
Inasaidia urahisi wa kumeza chakula na huboresha uwezo wa
macho kuona. Kwa wenye uzito
uliopitiliza na unene mkubwa, bamia hupunguza lehemu na kusaidia kukabiliana na
magonjwa mbalimbai.
Ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya
kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi mara kwa mara na hutibu pumu pia. Kwa wanaoitumia mara kwa mara, huongeza kinga
ya mwili.
Bamia ina wingi wa virutubisho vinavyosaidia kuimarisha afya
ya nywele. Kwa wanaofanya kazi za nguvu
au mazoezi mazito, bamia inasaidia kupunguza uchovu wa mwili na msongo wa
mawazo.
Bamia inasaidia kusafisha damu, kuponya mafua, kuondoa sumu
mwilini na hutibu vidonda vya tumbo. Kwa
watoto mboga hii ina faida chungu nzima.
Bamia inasaida kukabiliana na anemia, inazuia
utapiamlo huku ikiimarisha mifupa.
Ukiila kwa mpangilio mzuri itakusaidia kuongeza kinga dhidi ya
maambukizi ya figo, saratani pamoja na pumu.
No comments:
Post a Comment