Wakati ulaji wa vitu vyenye sukari kwa wingi ni hatari kwa
afya ikiwamo kuoza meno, lakini kwa tende ni tofauti kwa sababu tunda hili
huzuia uozaji wa meno.
Na hii ni kutokana tunda hili kusheheni vitamin na madini
mbalimbali yakiwamo ya chuma na nyuzinyuzi ambazo husaidia mmeng’enyo wa
chakula ambao husaidia kufikisha gastrointestinal system na kuupa mwili
nguvu. Ukila tende, mwili utapata nguvu
na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubusho
vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’, ambayo husaidia
kupata faida zaidi.
Tende imesheheni protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na
C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili, ndiyo maana kwa
wale wanaofunga saumu, inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili
kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima.
Hata hivyo, ulaji wa tende mara kwa mara huufanya mwili wako
upate aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, zinazopatikana kwenye
tende kwani ina kiasi kidogo cha mafuta na haina lehemu.
Watafiti wamegundua kuwa ulaji wa kiasi wa potasiam husaidia
kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi, lakini tunda hilo husaidia kupunguza
lehemu huku likiwa na madini aina ya potasiam na kiasi kidogo cha chumvi, madini
hayo husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu.
Tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo,
ulaji wa tunda utakusaidia kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo au kupata
kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia, lakini ndani ya tende
kuna virutubisho vya amino acid ambavyo ni muhimu mwilini. Kwa watu wenye ugonjwa wa anemia, wanaweza
kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha
madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini.
Kwa watu wenye tatizo sugu la ukosefu wa choo, loweka tende
za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya
maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo
kitafunguka na kuwa laini.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya lishe wanashauri kuwa
unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodaiwa kuongeza
nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha.
Kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa
kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment