Pera ni miongoni mwa matunda yenye faida kubwa kwenye mwili
wa binadamu kwa sababu vitamin C inayopatikana ndani ya tunda hilo, ni sawa na
mara nne zaidi ya ile inayopatikana kwenye chungwa. Na kwa wagonjwa wa kisukari, wanashauriwa kulila
mara kwa mara tunda hilo kwani lina kirutubisho chenye kinga dhidi ya sukari na hii ni kutokana kuwa na nyuzinyuzi (fibre).
Fibre ni muhimu katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu
na pia ni muhimu katika kuusafisha mfumo wa usagaji.
Pera ni zuri kwa wajawazito kwa sababu lina folic acid au
vitamin B-9 ambayo husaidia kujenga mfumo wa fahamu kwa mtoto aliyopo tumboni
pamoja na kuboresha uwezo wa kuona.
Pia tunda hili lina virutubisho mbalimbali ikiwemo vitamin
B2, E na K pamoja na madini ya chuma, ‘copper’, ‘potassium’ na ‘manganese’. Utafiti uliofanywa mwaka 1993 na kuchapishwa
katika Jarida la Journal of Human Hypertension unaeleza kuwa pera hupunguza
kiwango cha msukumo mkubwa wa damu ndani ya mwili kutokana na madini ya potassium
na vitamin C ambayo husaidia kuweka sawa msukumo wa damu ndani ya mwili. Hata hivyo, madini yaitwayo Folate ambayo
hupatikana katika tunda hili husaidia kurutubisha mayai ya uzazi na kuimarisha
uwezo wa mtu kuona kama ilivyo kwa karoti ambayo inasifika kwa kuwa na uwezo wa
kuimarisha uwezo wa kuona. Vitamin B3,
Vitamin B6 zilizopo ndani ya tunda hili ni muhimu katika kuimarisha afya ya
akili ya mwanadamu huku madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera husaidia
kurekebisa shinikizo la damu.
Mapera yana madini ya shaba ambayo ni mazuri katika
kurekebisha utendaji wa kazi ziitwazo thyroid na kwa kawaida tezi za thyroid
zisipofanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo ya afya kwa binadamu.
Wataalam wa masuala ya lishe wanashauri kutumia kula pera
baada ya kazi nzito na hiyo itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako
kupumzika.
Kwa wale wanaohitaji kuwa warembo, pera huzuia
kuzeeka kwa ngozi, kutoka na Vitamin zilizopo katika tunda hilo ambazo husaidia
kuondoa sumu mwilini na kuikinga ngozi yako dhidi ya mikunjo na kuchakaa.
No comments:
Post a Comment