Utafiti wa kisayansi uliofanyika unadhihirisha wanawake hasa
walio vunja ungo wapo katika hatari ya kupata maradhi ya UTI ukilinganisha na
wanaume.
Inaelezwa mambo yanayochangia kuugua ugonjwa huo ni urethra
kuwa fupi. Urethra ni mrija unaotoa
mkojo kutoka kwenye kibofu kupeleka nje.
Na mrija huo upo karibu na njia ya haja kubwa, hali ambayo hurahisisha
uwezekano wa bakteria kuingia katika mfumo wa mkojo na kusababisha maradhi ya
UTI.
Hatari ya UTI
UTI ni moja ya maradhi hatari hasa yanapowakumba
wajawazito. Utafiti unaonesha takribani
asilimia 40 ya wanawake wanaishi na UTI ambayo haijatibiwa na huwasababishia
wapate matatizo mbalimbali yanayohatarisha maisha yao na ya mtoto wakati na hata baada ya ujauzito.
Sababu zinazomfanya
mjamzito kuwa katika hatari ya kuugua UTI
Kutoweza au kupoteza uwezo wa kukamilisha haja ndogo
kikamilifu, matatizo katika mirija ya mkojo yanayotokana na mawe katika figo,
kukunjamana kwa mirija ya urethra na ureta, mimba kugandamizwa ureta pamoja na
matatizo katika mfumo wa fahamu, kushuka kwa nguvu kinga ya mwili, hali ambayo
huuweka mwili katika hatari ya kushambuliwa na maradhi mbalimbali. Ugonjwa wa kisukari pamoja na vipimo vya
hospitali visivyo salama anavyohudumiwa mjamzito huweza kuchangia maradhi hayo
na kuvimba kwa kuta za urethra.
Mambo mengine yanayochangia ni pamoja na kushuka kwa kinga
ya mwili, ujauzito kukandamiza mirija ya mkojo na kibofu. Bakteria wanaopanda kutoka kwenye mrija
unaotoa mkojo nje, yaani urethra na kuingia kwenye kibofu kisha kuzaliana. Hali hii husababisha UTI kwenye kibofu.
Sababu nyingine ni pale bakteria wanapotoka kwenye mfumo wa damu na kuelekea kwenye figo.
Mfano wa bakteria hawa ni Escherichia coli, proteus,
pseudomonas, Klebsiella na Staphylococcus hasa kwa wenye ugonjwa wa kisukari.
Sehemu za mfumo wa
mkojo zinazoathiriwa na UTI
Mrija unaosafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu kuelekea nje
unapovimba, husababisha urethritis.
Kuvimba kwa kibofu husababisha cytisis. Kuvimba kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo
kupeleka kwenye kibofu yaani ureters husababisha ureteritis na kuvimba kwa figo
husababisha pyelonephritis.
Namna ya kujitambua
kuwa tayari una UTI
Mtu aliye na maambukizi ya UTI mara nyingi huugua homa mara kwa mara na hupatwa na maumivu ya mgongo
hasa eneo la kiuno, kujisikia kichefuchefu na kutapika hasa wakati bakteria
wanapoanza kushambulia kwenye figo, kupata hamu ya kukojoa mara kwa mara,
maumivu ya kichwa, uchovu wa mwili mzima, maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa
mkojo uliochangamana na damu na usio na harufu ya kawaida, maumivu wakati wa
tendo la ndoa na maumivu sehemu za kibofu.
Unapopatwa na dalili hizo, muone daktari mapema.
Matatizo
yanayosababishwa na UTI wakati wa ujauzito
Ugonjwa huo ni hatari kwa mjamzito kwani unaweza
ukasababisha mimba kutoka kama hautatibiwa mapema.
Na wakati mwingine husababisha mjamzito akajifungua mtoto
kabla ya muda na wengine hujikuta wakijifungua
mtoto akiwa na uzito mdogo wa chini ya uzito wa kawaida wa kilo 2.5
yaani njiti.
Lakini wapo ambao pia huwasababishia mtoto akafia tumboni
pamoja na kupungukiwa damu na maji.
Namna ya kujikinga na
UTI
Ili kujikinga na maradhi hayo, madaktari wanashauri mtu
anywe maji ya kutosha, kwa siku isiwe chini ya lita moja na nusu. Pia aepuke kula vyakula vyenye sukari nyingi
ikiwamo kunywa pombe, chocolate na vyakula vyenye kahawa.
Inashauriwa kujenga tabia ya kukojoa mara ubanwapo na
mkojo. Kwa kufanya hivyo kutasaidia
kupunguza mkojo. Awahi kwenda kujisaidia
badala ya kuubana ni hatari.
Inashauriwa kujenga tabia ya kuoga na kukojoa kabla na baada
ya tendo la ndoa. Kufanya hivyo husaidia
kuondoa bakteria walioko sehemu za siri.
“Epuka tendo la ndoa kama upo katika matibabu ya UTI na
baada ya kukojoa usifute bali kausha na sehemu zako za siri ziweke safi na kavu
muda wote na kama utazifuta hakikisha unafuta mbele kuelekea nyuma,”
inaelekezwa.
Ni vizuri kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana
na hakikisha zile uzivaazo ni safi. Nguo
za ndani aina ya kotoni zinapendekezwa zaidi kutumika sambamba na kula vyakula
vyenye vitamin C kama matunda aina ya machungwa huwa na asidi ambayo husaidia
kuondoa bakteria.
No comments:
Post a Comment