Friday, January 5, 2018

TIKITIMAJI HUIMARISHA FIZI NA KUHARAKISHA MMENG’ENYO WA CHAKULA


Tikitimaji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi nchini likiwa na virutubisho vingi vyenye faida kubwa mwilini.

Tikiti ni chanzo cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga, calcium, phosphorus, potassium, magnesium, carotene, chuma, vitamin A, B6 na C. ni tunda linalopatikana kwa urahisi nchini.

Tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Iycopene kuliko matunda au mboga zozote za majani.  Wengi hula tunda hili bila kufahamu faida lukuki ilizonazo.  Iwe shereheni au hotelini na wakati mwingine nyumbani, tikitimaji ni rafiki wa afya.

Wengi wanaokula tunda hili hutema mbegu zake lakini zikitafunwa na kumezwa faida zake ni kemkem kwa afya ya mlaji.  Wataalam wa masuala ya lishe wanasema mbegu za tikitimaji zinaprotini nyingi hivyo kuzitafuna kunaweza kumpatia mlaji chanzo cha virutubisho hivyo.

Licha ya kupatikana kwa bei nafuu, huuzwa sehemu tofauti kwenye baadhi ya maeneo huuzwa hata kwa vipande hivyo kutoa unafuu kwa wasiotaka tunda zima.  Ingawa haishauriwi kula matunda yaliyomenywa, vipande vya tikitimaji huuzwa barabarani pia.

Hata hivyo, tikitimaji lina faida nyingi mwilini zinazotokana na wingi wa maji iliyonayo.  Wataalam wanaeleza kwamba asilimia 92 ya tunda hilo ni maji.  Ni muhimu kwa afya ya meno na fizi.  Linakinga uharibifu wa seli huku likisaidia uyeyushaji wa protini kuwa nishati na hurahisisha mzunguko wa damu mwilini.

Mafuta yaliyopo kwenye mbegu hizo hayana lehemu kwa kiwango kikubwa hivyo kutosababisha kuziba kwa mishipa ya damu hivyo kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Mbegu za tikitimaji ni nzuri kwa afya.  Zinaongoza kwa kuwa na viinilishe ikilinganishwa na mbegu nyingine.

Vilevile huondoa sumu mwilini na kwa mwanaume anayekula mbegu zake husaidia kuongeza nguvu za kiume.  Huimarisha kinga za mwili na kuharakisha kupona kwa vidonda na majeraha.

Ni wakati wako sasa kulifanya tunda hili kuwa sehemu ya chakula chako cha kula siku na kama ulikuwa hulipendi, ni vyema ukabadili msimamo na kuanza kulizoea.
Share:

No comments:

Post a Comment