Muwasho ndani ya koo unatokana na sababu mbalimbali japo kwa
kiasi kikubwa unachangiwa na mzio (aleji) wa vitu ikiwamo ile itokanayo na
baadhi ya vyakula.
Kupitia mzio unaotokana na vyakula, hutokea pia wakati kinga
ya mwili inapambana na vimelea vilivyopo kwenye vyakula tunavyokula vyenye
kuhatarisha afya zetu.
Kwa kawaida, kinga ya mwili hupambana na vimelea hivi vya
maradhi muda mfupi baada ya kula vyakula vyenye vimelea vya maradhi.
Lakini kwa watu wengine, mzio unaweza kutokea hata siku
kadhaa baada ya kula vyakula hivyo.
Mzio unaweza kuwa wa kawaida ukiambatana na dalili chache
zikiwamo za muwasho ndani ya koo au mdomoni.
Hata hivyo, mara chache inaweza kutokea kuleta madhara
makubwa zaidi kiafya. Hivyo ni vyema
kuwa makini katika ulaji wa baadhi ya vyakula kama ngano, baadhi ya aina za
kunde, baadhi ya nyama mbichi, mayai na hata maziwa.
Vyote hivyo mara nyingi husababisha mzio kwa walio wengi.
Mzio hutokea pia kutokana na matumizi ya aina mbalimbali za
dawa ambazo husababisha muwasho ndani ya koo.
Wengi wanaoshambuliwa na mzio unaotokana na matumizi ya dawa
hasa kiantibayotiki kama vile penicillin zinazotumika kuzuia maambukizi ya
vimelea mbalimbali.
Mzio huu unapotokea huleta ishara mbalimbali mwilini ikiwamo
muwasho ndani ya koo.
Mtu anapokuwa na mafua makali hasa wakati wa baridi, maumivu
na muwasho ndani ya koo yanaweza kuongezeka mara dufu vikiambatana na hali ya
homa na maumivu ya kifua.
Muwasho huu unaweza kudumu kwa muda usipopatiwa tiba na
unaweza kuwa hatari kwa afya.
Muwasho ndani ya koo pia unasababishwa sana na maambukizi ya
kibakteria na yale yatokanayo na baadhi ya virusi vya maradhi mbalimbali.
Kuna maambukizi ya maradhi ambayo mara nyingi hutokea kooni
ambayo kwa kitaalamu yanaitwa “streptococall” au “strep throat”.
Maambukizi haya yanapotokea yanaweza yakaambatana na vidonda
kwenye koo ambavyo wengi pia huwa wanavipata (tonsillitis) yakiambatana na
muwasho ndani ya koo hatimaye kuongezeka na kuleta maumivu makali kwenye
koo. Baadhi ya virusi vinavyosababisha
mafua pia vinaweza kuleta muwasho ndani ya koo.
Ni Dhahiri kuwa, kila mmoja anafahamu umuhimu wa maji kwenye
maisha yetu ya kila siku na hasa kwa afya.
Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha maji unasababisha kwa
kiasi kikubwa sana tatizo la muwasho ndani ya koo. Upungufu wa maji mwilini unatokea pale ambapo
mwili unapoteza kiasi kikubwa cha maji kuliko kile kinachoingia na mara nyingi
hali hii hutokea wakati wa joto sana, baada ya kufanya mazoezi ya mwili au hata
wakati wa homa. Upungufu wa maji mwilini
unatokea pale ambapo mwili unapoteza kiasi kikubwa cha maji kuliko kile
kinachoingia na mara nyingi hali hii hutokea wakati wa joto sana, baada ya
kufanya mazoezi ya mwili au hata wakati wa homa. Upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha
kukauka kwa mdomo, japo hali hii huwa ni ya muda kwa sababu mdomo na koo
havipati mate ya kutosha kutokana na upungufu wa maji mwilini na hivyo
kupelekea kupata muwasho ndani ya koo.
Utendajikazi wa madawa mwilini pia unasababisha muwasho
ndani ya koo.
Baadhi ya madawa yanaweza kusababisha kikohozi kikavu na
muwasho ndani ya koo ambayo hayatokani na aleji zinazotokana na dawa. Watu wanaotumia baadhi ya dawa za shinikizo
la damu wanapaswa kutambua kuwa dawa hizo zinaweza kusababisha kikohozi kikavu
na muwasho ndani ya koo wakati wa utendaji kazi wake mwilini. Kwa kawaida dalili hutokea mara tu baada ya
kutumia dawa hizi na mara zote haziambatani na dalili zingine tofauti na
muwasho ndani ya koo na kikohozi kikavu.
Kwa kawaida huwa si rahisi kugundua kama muwasho ndani ya
koo umetokana na baadhi ya magonjwa au ile inayotokana na baadhi ya vyakula,
hivyo ni vyema kuzitambua dalili zake ndipo utagundua kama muwasho huo
umetokana na vyakula au maradhi mengine.
No comments:
Post a Comment