Tuesday, August 25, 2015

NAMNA YA KUPATA MTOTO WA KIUME

son

Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100.  Bali ni njia ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.

Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto.  Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kama ikifuatwa vizuri basi huweza kuwa na mafanikio.

Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu ya XX na ya kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.

Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume.
Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi mkubwa lakini hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi, lakini huishi kwa muda mrefu.  Kwa kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.

Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa, ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye kinyume cha hatua hizi.

Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku ambayo yai la kike linatoka.  Hiki ni kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume hivyo mimba huweza kutungishwa.

Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa kuvutika hufanana kama vile wa mayai ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.

Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute.  Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara nyingi ukiwa umelala.

Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi kipindi cha ovulation.  Ni vizuri chati hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa pamoja.

Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki.  Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana.  Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00 usiku.

Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la ndoa.  Ni vizuri kufanya tendo la ndoa kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation.  Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.

Hatua ya tatu
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama.
Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume humwagwa karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.

Hatua ya nne
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi (alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi.  Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa mbegu ya kiume.

Hatua ya tano
Hii ni kwa upande wa mwanaume.  Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na kubana.  Unapaswa kuvaa chupi au nguo ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba.  Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu za kiume.  Joto pia hupunguza ubora na utengenezaji wa mbegu za kiume.

Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya tendo la ndoa.  Hii huongeza nguvu ya mbegu za kiume aina Y.

Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo.  Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na siku ya tendo.  Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.  Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji vyenye glukosi.

Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa, vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza.

Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya kunde kupitia kiasi.

Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe, hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili.  Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.

Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa tendo lenyewe.  Lengo ni kuwa na utulivu wa kimwili na kiakili pia.  Hii itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe.


Share:

Friday, August 14, 2015

JE,UKO HATARINI?


Joe alikuwa amechoka na kuishiwa na pumzi.  Hata kazi rahisi kabisa kama vile kutembea kuzunguka nyumba au kwenda kwenye gari, ilimfanya apumue kwa shida.  Alikaa ofisini kwa daktari, akiwa amekata tamaa na kufadhaika.  Alikuwa hajapunguza uzito tangu alipokuja miezi miwili iliyopita.  Kufanya mambo yawe mabaya zaidi, alikuwa bado anavuta sigara, na kiwango cha sukari katika damu yake kilikuwa kikubwa.  Lakini alikuwa bado hawezi kuacha kula donati zenye sukari ambazo alikuwa anazila kila asubuhi, akishushia na kahawa yenye sukari au vinywaji vya kola.  Kwa sababu ya kisukari chake namba 2, kuvuta sigara, unene kupita kiasi, na maisha ya kukaa bila kazi za kutumia nguvu, Joe alikuwa ameshikwa na ugonjwa wa moyo miaka miwili kabla, akiwa na miaka 35.  Ulikuja kwa nguvu na kumwacha na kovu kubwa katika msuli wa moyo wake na tatizo la kushindwa kwa moyo kufanya kazi vizuri.

Akiwa na haya kidogo, Joe alielezea wasiwasi wake kwa daktari wake.  “Ndiyo Daktari, nilikuwa najua kuwa hutafurahia kushindwa kwangu kupunguza uzito, na kwa kuwa bado ninavuta sigara kidogo naomba unielewe, sivuti mpaka mapafuni!  Samahani daktari; sipendi kukuangusha.”
Daktari alimtia moyo kwa upole ili azidi kujitahidi, alieleza kuwa kutokana na kasoro ya kusukuma damu iliyotokana na ugonjwa wa moyo, kisukari kisichodhibitiwa, na uvutaji wa sigara, pamoja na uzito wake uliopita kiasi, asipofanya mabadiliko makubwa atakufa akiwa kijana.

Jibu la Joe lilikuwa la ajabu, “Je daktari, inawezekana kubadilishwa moyo?  Nimesikia huwa unabadilishwa.  Je, ninaweza kupata moyo mwingine?”

“Laiti ingekuwa rahisi na sahihi kiasi hicho,” daktari wake alisema.  “Mioyo inayotolewa kwa ajili ya kubadilisha ni adimu sana, na bado kuna kutumia dawa kwa miaka mingi baada ya hapo.  Hiyo ni njia ya mwisho inayoweza kusaidia, lakini inayowezekana kwa watu wachache tu.  Inakupasa kubadili mtindo wa maisha tena mara moja.”  Hatimaye Joe alielewa hatari ya hali yake na kuanza kubadili namna alivyokuwa anaishi.


Mamilioni ya watu huwa wanahangaika na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ulimwenguni kote kama Joe:  Magonjwa ya moyo, saratani, magonjwa ya njia ya hewa, na kisukari.  Yote haya yanasababishwa na mambo makuu manne:-  Matumizi ya tumbaku, kutoshughulisha mwili, pombe na vyakula visivyofaa.  Unaweza kuwa hatarini bila kujua.
Share:

Monday, July 13, 2015

PINEAPPLE (Ananas comosus Mill)


pineapple plant
The much-loved pineapple is tropical, spiny-leaved shrub that belongs to the plant family Bromeliaceae.  The numerous leaves are linear-lanceolate or sword-shaped and are 1-1.5 m long and 5-7 cm. wide.  The leaf margins are spiny-toothed, rigid and concave on the upper side.  The small stalked red flowers unite at the base and mature into the fleshy fruit, the pineapple, which is 20 cm.  or more in length.  The plant is commonly cultivated in tropical countries.

Medicinal Use
·         Bronchitis.
·         Sore throat.
·         Constipation, reduction of fever, for digestion, treatment of the bladder, prostate, urethra, amenorrhoea or absence of menstruation, rheumatism, arthritis, oedema, jaundice, neurasthenia or weakness of the nervous system, melancholia or extreme depression, nephritis or inflammation of the kidney, and loss of memory.
·         Expels worms, and kills intestinal parasites.
·         Gonorrhea, which is a sexually transmitted disease and anuria or the inability to urinate.

How to use
For bronchitis the pineapple is sliced and covered with honey and then boiled to make syrup.  Two to three spoonfuls a day is a good expectorant.

For sore throat, the natural ripe fruit is eaten, or the juice is drunk.

The pulp or the juice is recommended for constipation, reduction of fever, for digestion, treatment of the bladder, prostate, urethra, amenorrhoea or absence of menstruation, rheumatism, arthritis, oedema, jaundice, neurasthenia or weakness of the nervous system, melancholia or extreme depression, nephritis or inflammation of the kidney and loss of memory.

The decoction of the leaves of the plant is used for expelling worms, and to kill intestinal parasites.

The leaves mixed with the unripe fruit, is indicated for gonorrhea, a sexually transmitted disease and anuria or the inability to urinate.

Parts used
the leaves and ripe and unripe fruit.

Dose
For leaves and unripe fruit, use 20 to 30 grams for 1 litre of water.  Use 4 to 5 cups a day.  The ripe fruit may be used abundantly.

Caution

Pregnant women should not use the tea of the leaves or the unripe fruit.
Share:

ELEPHANT’S FOOT (Amorphophallus campanulatus Blume)


elephant's foot plant
The plant is a tuberous herb cultivated throughout the country.  The large, dark brown, dorso-vertrally compressed and succulent corm, which is 20-25 cm.  in diameter, is used as a vegetable.  The plant belongs to the plant family Araceae.  The leaves forming a rosette at the terminal end, are compound, large with stout 60-90 cm. long petioles.  The spadix inflorescence, 20 cm. long, bears the male and female flowers, which are protected by a large, broad spathe which is about 25 cm. long.

Medicinal Use
·         Relieves pain
·         Promotes menstruation
·         Helps in indigestion.
·         Helps in reducing inflammation.
·         Cures piles.
·         Helps in removing phlegm.
·         Expels worms.
·         Elephantiasis.
·         Tumours.
·         Cough, bronchitis, asthma.
·         Helps in expelling gas from the stomach.
·         Anaemia.

How to use
The consumption of the boiled corm controls and cures the conditions and ailments listed under Medicinal use

Parts used
The underground corm.

Dose

As recommended above.
Share:

Tuesday, June 30, 2015

UGONJWA WA PUMU NA HATARI ZAKE

PUMU
Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko uvimbe sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitishia hewa (bronchi oles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii na kuwa na ute mzito hivyo kupungua kwa njia ya kupitishia hewa.
Hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Tatizo hili linaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.
Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hewa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease .
Mtu aliye na pumu huwa na kipindi ambacho hawi na tatizo la pumu mpaka pale mwili unapochokozwa na kuingia katika hali hiyo. Wakati huo wote cha maisha yake kinachotokea ni kutulia tu mpaka pale inapotokea uchokozi mwilini.
Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili, iko pumu ya ghafla ijulikanayo kitabibu kama Acute asthma. Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika wakati wa shambulio na usio wa shambulio.
Kundi jingine ni Pumu sugu (Chronic Asthma). Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu njia za hewa huzidi kuwa nyembamba na kusinyaa zaidi.
Aina za pumu
Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni inayobadilika, isiyobadilika, ya mazoezi na inayosababishwa na kazi.
Pumu inayobadilika (brittle asthma): Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ya ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili.
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.
Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla (asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.
Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na matumizi ya dawa kadhaa, zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka na anaweza kupoteza maisha.
Share:

Monday, June 29, 2015

MAZOEZI YA MIFUPA

borne exercise
Kama ilivyo misuli ya mwili, mifupa nayo ni tishu zenye uhai zinazofaidika kwa mazoezi ya mwili. Mazoezi huimarisha mifupa na kuifanya iwe na nguvu, iwe na umbo zuri pamoja na ujazo mzuri.
Kwa kawaida mifupa huendelea kukua na kuwa imara katika miaka ya utotoni hadi wakati wa ujana kabla ya miaka 30. Baada ya kipindi hiki cha umri, mifupa taratibu inaanza kupoteza uimara wake na katika kipindi hiki ndipo mazoezi yanapohitajika zaidi. Mazoezi yanasaidia kuimarisha misuli inayojishikiza katika mifupa na kuwa na stamina, mambo ambayo yanapunguza uwezekano wa mtu kuanguka ovyo na kuvunjika mifupa.
Mazoezi yanayoimarisha afya ya mifupa ni muhimu hasa kwa wagonjwa wenye udhaifu wa mifupa, watu wanaofanya kazi za kukaa ofisini muda mrefu, wazee na wanawake waliokoma kupata siku zao za hedhi.
Mazoezi mazuri kwa ajili ya uimara na afya ya mifupa ni yale yanayohusu na mwili kubeba uzito.
Mifano ya mazoezi haya ni kama vile kubeba vitu vizito, kupiga pushapu, kupanda milima, kupanda ngazi, kukimbia taratibu, kutembea kwa muda mrefu pamoja na kucheza muziki unaohitaji minenguo ya aina mbalimbali.
Mazoezi haya pia, yanaweza kuchanganywa na mazoezi ya kuimarisha afya ya moyo na misuli. Mazoezi kama vile kuogelea, kuruka kamba na kuendesha baiskeli yanaweza pia kusaidia moyo na misuli kuwa na nguvu.
Kabla ya kuanza mazoezi yanayoimarisha mifupa, ni jambo la busara kupata ushauri wa kitabibu. Jambo hili ni muhimu hasa kwa watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama vile udhaifu wa mifupa, maumivu ya mgongo, kisukari, matatizo ya moyo na figo, shinikizo la damu, kifafa na unene wa kupindukia.
Watu wazima wenye miaka zaidi ya 40 ambao kwa kawaida hawana mazoea ya kufanya, nao wanatakiwa kupata ushauri wa kitabibu kabla ya kuanza mazoezi ya kuimarisha mifupa yao. Mazoezi ya kuimarisha mifupa sharti yafanyike kila siku au mara tatu katika kipindi cha juma moja na yasiwe chini ya dakika 30 kwa siku.
Shirika la Afya Duniani (WHO) katika chapisho lao la mwaka 2010 linalozungumzia umuhimu wa mazoezi kwa afya (GRPAH), linapendekeza watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, wafanye mazoezi mepesi angalau kwa dakika 150 au mazoezi mazito angalau kwa dakika 75 ndani ya juma moja. Ni vizuri kusikiliza kengele ya mwili wako hasa pale unapoanza mazoezi haya.
Pale unapoanza mazoezi unaweza kuhisi maumivu ya misuli, hivyo basi usijilazimishe kuendelea. Simamisha mara moja mazoezi yako hasa pale unapohisi maumivu ya kifua wakati wa mazoezi na wasiliana na daktari.
Kwa watu wanajali afya ya mifupa yao, pamoja na mazoezi, ni jambo la busara kujiepusha na matumizi ya tumbaku, ulevi wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya.
Inashauriwa pia kupata mlo kamili hasa wenye kiasi cha kutosha cha madini ya kalisi (calcium) na vitamini mbalimbali. Dagaa na samaki tunaoweza kuwatafuna na mifupa yao, korosho pamoja na kunywa maziwa kwa kiasi, ni njia bora za kutupatia madini ya kalisi.


Share:

MAYAI YASIPOIVA NI HATARI!

Mayai hayajaiva

Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.
Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.
Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.
Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.
Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.
Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.
Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.
Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.
Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.
Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.
Wataalamu wanasemaje?


Share: